Rais Wa Msumbiji Filipe Nyusi na Mkewe Isaura Nyusi wamelazimika kujitenga kwa lazima baada ya Kupatikana na Virusi vya Covid-19.
Taarifa Zinabaini kwamba, Rais Filipe na Mkewe Isaura walipatika na Virusi hivyo baada ya kupimwa ikuluni. Bwana Filipe alikuwa amejishughulisha na shughuli hapo nyuma ambapo inaaminika Wenda kaambukizwa na virusi hivyo kutokana na shughuli hizo za awali.
Wawili hao walilazimika kujitenga kwa lazima huku wakisubiri kupona. Rais na mkewe walionesha dalili za Virusi vya Covid-19 ambapo ililazimu kupimwa na hatimaye virusi vya Covid-19 kuonekana.
Nchi ya Msumbiji ni miongoni mwa mataifa ulimwenguni ambayo imekumbwa na janga hili la covid-19. Taarifa zinabaini kwamba, watu waliothibitishwa kupatikana na virusi vya Covid-19 nchini imetimia 193,000 na vifo vipatao watu 2031 vimerekodiwa.
Fuata kwenye tovuti stateupdate.co.ke kupokea habari Zaidi.